Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 06:40

Vuguvugu la uchaguzi DRC, Wakongo milioni 44 wajiandikisha kupiga kura


Félix Tshisekedi kushoto, na Martin Fayulu (Président RDC)
Félix Tshisekedi kushoto, na Martin Fayulu (Président RDC)

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa nne tangu kuanza mfumo wa vyama vingi miaka 20 iliyopita. Wakongo milioni 44 wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi wa kumchagua rais, wajumbe wa bunge la Taifa, wa mabunge ya majimbo na kwa mara ya kwanza madiwani wa mabaraza ya miji.

Katika uchaguzi wa rais kumekua na wagombea 28 lakini kufikia siku za mwisho idadi imepunguka na kufikia 19 ambapo rais Felix Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60 akigombania mhula wake wa pili, na mpinzani aliyemshinda wakati wa uchaguzi wa 2018, Martin Fayulu mwenye umri wa miaka 67 akijaribu kutetea haki aliyopoteza.

Kastika uchaguzi wa bunge la taifa kuna wagombea elfu 20,300 kwa ajili ya viti 500 vya baraza kuu la bunge, ikiwa idadi kubwa kuwahi kushuhudiwa.

Uchaguzi huu ni muhimu kwani itaweza kuwa ni mara ya pili kukabidhiana madaraka kati ya rais na rais tangu nchi hii kujinyakulia uhuru kutoka Ubelgiji mwezi Juni 1960.

Hata hivyo uchaguzi huu umegubikwa na wasi wasi mkubwa wa kuwepo na uwazi na haki na hasa baada ya tume ya Umoja wa Ulaya kuondoa ujumbe wake wa wafuatiliaji uchaguzi, na kutokana na vile maelfu na maelfu ya wakazi katika majimbo yanayokumbwa na vita hawataweza kushiriki kwenye uchaguzi huo kutokana na ukosefu wa usalama.

Tume Huru ya Uchaguzi ya DRC, CENI, inayo ongozwa na Denis Kadima inajitetea kwamba uchaguzi utafanyika kwa njia huru na haki na uwazi. Kadima aliwambia waandishi Habari mjini Kinshasa kwamba Utaratibu unaendelea vizuri licha ya changamoto chungu nzima walizokumbana nazo. Anasema wako tayari kabisa kuandaa uchaguzi ambao utakua wa kuaminika licha ya kwamba kuna wengi wanaotilia shaka kazi zao.

Umoja wa Mataifa katika wiki ya mwisho imeitikia wito wa Kinshasa na kupeleka ndege mbili za kijeshi za kusafirisha mizigo ili kusaidia kusambaza vifaa vya upigaji kura.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Kinshasa, DRC

Forum

XS
SM
MD
LG