Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:10

HRW inasema Demokrasia nchini DRC imekuwa ikirudi nyuma kuelekea uchaguzi


Human Rights Watch (HRW), shirika la kutetea haki za binadamu
Human Rights Watch (HRW), shirika la kutetea haki za binadamu

Rais Felix Tshisekedi aliingia madarakani mwaka 2019 baada ya kampeni ya kukosoa rekodi ya haki za binadamu ya mtangulizi wake Joseph Kabila, miongoni mwa mambo mengine. Lakini matukio kadhaa ya hivi karibuni yamezua wasiwasi kuhusu rekodi ya Rais Tshisekedi mwenyewe.

Demokrasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikirudi nyuma kuelekea uchaguzi mkuu siku chache zijazo, kulingana na watetezi wa haki, wakati waandishi wa habari maarufu wakiteseka gerezani, na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani bado hayajatatuliwa.

Rais Felix Tshisekedi aliingia madarakani mwaka 2019 baada ya kampeni ya kukosoa rekodi ya haki za binadamu ya mtangulizi wake Joseph Kabila, miongoni mwa mambo mengine.

Lakini matukio kadhaa ya hivi karibuni yamezua wasiwasi kuhusu rekodi ya rais mwenyewe. Waziri wa zamani aliyegeuka kuwa mwanachama wa upinzani alikutwa amekufa katika mji mkuu wa taifa hilo la Afrika ya Kati, Kinshasa mwezi Julai.

Ramani ya jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nchi zilizo jirani nae.
Ramani ya jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nchi zilizo jirani nae.

Miezi michache baadaye, mmoja wa waandishi wa habari maarufu wa Kongo alifungwa jela baada ya mamlaka kumshutumu kueneza habari za uongo kuhusu mauaji hayo. “Hizi ni ishara za kupungua kwa nafasi ya demokrasia”, alisema mtafiti wa haki za binadamu, ambaye aliomba jina lake lisitajwe. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatarajiwa kufanya uchaguzi Desemba 20.

Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60 atawania muhula wa pili madarakani. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeonya leo Jumamosi kwamba limerekodi mapigano na ghasia nyingine kati ya wafuasi wa vyama vinavyohasimiana, matukio ambayo yanaweza kuhujumu uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG