Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:48

Tume ya uchaguzi nchini DRC yatangaza orodha ya muda ya wagombea urais 24.


Mshindi wa tuzo ya amani ya Nober Daktari Denis Mukwege, baada ya kutangaza kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi wa Disemba, Oktoba 2, 2023.
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nober Daktari Denis Mukwege, baada ya kutangaza kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi wa Disemba, Oktoba 2, 2023.

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Ijumaa imethibitisha orodha ya muda ya wagombea 24 ambao wamejiandikisha kwenye uchaguzi wa rais wa tarehe 20 Disemba.

Wagombea hao bado wanahitaji kuidhinishwa na Mahakama ya Kikatiba, huku orodha ya mwisho ikitarajiwa kuchapishwa tarehe 18 Novemba.

Rais Felix Tshisekedi ambaye aliingia madarakani mwaka 2018, aliwasilisha fomu yake ya kuwania muhula wa pili wa miaka mitano mapema mwezi huu wa Oktoba.

Kutokana na upinzani uliogawanyika, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60 yuko “nafasi nzuri ya kushinda”, amesema mchambuzi wa siasa kutoka Congo Christian Mokela.

Kulingana na Mokela, upinzani wa kisiasa uliogawanyika utahitajika kuunga mkono mgombea mmoja ili kuweza kuwa na bahati ya kumshinda Tshisekedi.

Wapinzani wakuu wa Tshisekedi ni pamoja na Daktari Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Nobel, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga Moise Katumbi, na Martin Fayulu ambaye alishindwa katika uchaguzi wa 2018.

Forum

XS
SM
MD
LG