Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:39

Uganda yaongeza muda kwa kampuni ya Nigeria kuendelea kutafuta mafuta


Kinu cha mafuta cha Kingfisher nchini Uganda kinachoendeshwa na kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), Jan. 24, 2023. (AP Photo/Hajarah Nalwadda)
Kinu cha mafuta cha Kingfisher nchini Uganda kinachoendeshwa na kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), Jan. 24, 2023. (AP Photo/Hajarah Nalwadda)

Wizara ya mafuta ya Uganda imesema Jumamosi kwamba imeongeza muda wa leseni kwa kampuni ya Nigeria ya Oranto Petroleum Limited, kwa muda wa miaka miwili zaidi.

Hatua hiyo sasa itatoa nafasi kwa kampuni hiyo kuendelea kutafuta mafuta kwenye maeneo mawili yaliopo magharibi mwa nchi. Leseni hiyo inayojumuisha maeneo ya Ngassa Deep na Ngassa Shallow itaruhusu kampuni hiyo kutafuta na kuidhinisha shuguli za uchimbaji mafuta, kulingana na taarifa iliyotolewa Ijumaa jioni.

Uganda iligundua mafuta yanayofikia viwango vya kibiashara kwenye eneo la Albertine Graben, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hapo 2006, wakati ikipanga kuanza kuyauza kufikia 2025.

Forum

XS
SM
MD
LG