Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 17:10

Kundi la ADF ladaiwa kufanya mauaji Uganda

Wanamgambo wanaohusishwa na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State wamewachoma moto takriban raia 10 hadi kufa katika shambulizi katika mji wa kusini magharibi mwa Uganda, polisi wamesema Jumanne.

Wanamgambo hao kutoka kundi la ADF, moja ya wanamgambo walioua zaidi katika eneo lenye mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, walivuka mpaka na kushambulia kituo cha biashara cha Kamwenge, polisi wamesema.

“Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa washambuliaji 10 waliokuwa na bunduki aina ya SMG waliwashambulia na kuwachoma hadi kufa watu 10,” msemaji wa polisi mkoani humo Vincent Twesige amesema.

ADF kihistoria ni muungano wa waasi wa Uganda ambao kundi lake kubwa linajumuisha wenye msimamo mkali na kumpinga rais Museveni.

Forum

XS
SM
MD
LG