Allied Democratic Forces (ADF), iliundwa kama kundi la uasi dhidi ya Kampala katika miaka ya katikati ya 1990, na awali lilipambana na serikali ya Rais Yoweri Meseveni kutoka katika kambi zilizoko katika milima ya Rwenzori.
Siku ya Jumatatu majira ya saa nne usiku, kundi hilo la waasi liliivamia parokia ya Kyabandara katika wilaya ya Kamwenge Mgaharibi mwa Uganda, alisema mbunge Cuthbert Abigaba.
Washambuliaji hao walimuua diwani wa eneo hilo ambaye alikutwa kwenye mgahawa mdogo kando ya barabara alikokuwa akifanyakazi, akiwa na wateja wake wanne ambao walikuwa wameketi kwa ajili ya kupata chakula, alisema.
“Baada ya mauaji, waliuchoma moto mgahawa na pia kupora vitu katika maduka yaliyoko jirani kabla ya kukimbia” alisema Abigaba.
Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Deo Akiiki, alithibitisha shambulio hilo na kusema watatoa taarifa zaidi baadaye.
Baada ya kuundwa kwake, ADF hatimaye lilisambaratishwa na jeshi na waliobaki walikimbialia Mashariki mwa Congo ambako walianzisha mashambulizi mabaya katika maeneo yote yaliyoko huko Congo na Uganda.
Uganda ilianzisha kampeni ya anga na ardhini dhidi ya ADF nchini Congo Mwaka 2021.
Meseveni alisema operesheni hiyo ilifanikiwa kuuwa kundi kubwa la waasi wakiwemo baadhi ya makamanda.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters
Forum