Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:46

Mwanamke wa miaka 70 ajifungua mapacha Uganda


Jiji la Kampala Uganda
Jiji la Kampala Uganda

Mwanamke nchini Uganda mwenye umri wa miaka 70 amejifungua watoto mapacha, daktari wake alisema siku ya Alhamisi, katika kile ambacho mama huyo alidai kuwa ni muujiza.

Safina Namukwaya alielezea furaha yake ya kupata mapacha hao ambao walizaliwa siku ya Jumatano katika kituo cha matibabu katika mji mkuu wa Kampala, ambako alikuwa amepata matibabu ya uzazi.

"Haya ni mafanikio ya ajabu, kujifungua mapacha kwa mama mwenye umri mkubwa sana barani Afrika mwenye umri wa miaka 70," Daktari Edward Tamale Sali, ambaye alisimamia ujauzito wake na kujifungua, aliliambia shirika la habari la AFP.

Alisema mama na watoto -- mvulana na msichana wako na afya njema—lakini bado katika uangalizi katika Kituo cha Kimataifa cha Hospitali ya Wanawake na Kituo cha Uzazi ambacho alikianzisha.

"Hakuna jinsi ya kuelezea furaha yangu kwa sasa," alisema Namukwaya, ambaye anaishi eneo la vijijini vya Masaka takriban kilomita 120 Magharibi mwa Kampala.

"Nikiwa na umri wa miaka 70 ninaonekana ni mdhaifu, siwezi kupata mimba na kujifungua, au kutunza mtoto, na hapa kuna miujiza wa mapacha hao," aliliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Namukwaya alisema hapo awali alijifungua mtoto wa kike mwaka 2020, baada ya kukejeliwa kama "mwanamke aliyelaaniwa" ambaye hapo awali hakuwa anazaa.

Alisema mume wake wa kwanza alifariki mwaka 1992 na kumwacha bila watoto, na alikutana na mpenzi wake wa sasa mwaka 1996.

Lakini Namukwaya alionyesha kusikitishwa kwamba mpenzi wake hajamtembelea tangu alipofika hospitali kujifungua.

“Labda hajafurahishwa kwamba nilijifungua mapacha kwa sababu wanaume hawataki kujua umebeba zaidi ya mtoto mmoja tumboni kwa kuhofia majukumu yanayoambatana nayo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG