Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 08:09

Kampuni ya Afrika Kusini kutengeneza kingo za Uke za kujikinga na VVU


Mwelimishaji wa Taasisi ya Afya ya Uzazi akionyesha vifaa vya kupimia VVU. Picha na GULSHAN KHAN / AFP
Mwelimishaji wa Taasisi ya Afya ya Uzazi akionyesha vifaa vya kupimia VVU. Picha na GULSHAN KHAN / AFP

Kampuni ya Afrika Kusini itatengeneza kifaa maalum kinachoingizwa ukeni kwa wanawake ili kujikinga na maambukizi ya VVU, ambacho wataalam wa UKIMWI wanasema kitapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Baraza la Idadi ya Watu lilitangaza siku ya Alhamisi kuwa Kiara Health ya Johannesburg itaanza kutengeneza kifaa hicho kinachojulikana kama ‘silicone ring’ katika miaka michache ijayo, na kukadiria kuwa vifaa milioni moja vinaweza kutengenezwa kila mwaka.

Vifaa hivyo hutoa dawa ambayo husaidia kuzuia maambukiz ya VVU na vimeidhinishwa na karibu nchi kadhaa pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni.

Baraza ambalo lisilo la faida linamiliki haki za vifaa hivyo, ambavyo sasa zinatengenezwa na kampuni ya Uswidi. Mpaka sasa takriban pete 500,00 zinapatikana kwa wanawake barani Afrika bila gharama, zinazonunuliwa na wafadhili.

Ben Phillips, msemaji wa shirika la U.N. UKIMWI, alisema faida ya kifaa hicho ni kwamba inawapa wanawake uhuru wa kuitumia bila mtu mwingine kujua au kutoa ridhaa.

"Kwa wanawake ambao wapenzi wao hawatatumia kondom au kuwaruhusu kutumia dawa za kumeza (kuzuia VVU), hii inawapa chaguo jingine," alisema.

VVU vinabaki kuwa chanzo kikuu cha vifo miongoni mwa wanawake walio katika umri wa kuzaa barani Afrika na asilimia 60 ya maambukizi mapya ni ya wanawake, kulingana na takwimu za WHO.

Kifaa hicho hutoa dawa ya dapivirine kwa dozi za polepole zaidi ya mwezi mmoja. Kwa sasa inagharimu dola 12 hadi 16, lakini wataalam wanatarajia bei hiyo itashuka mara kitakapozalishwa kwa wingi barani Afrika.

Watengenezaji pia wanashughulikia toleo litakalodumu hadi miezi mitatu, ambalo linapaswa pia kupunguza gharama ya kila mwaka.

WHO imependekeza kifaa hicho kitumike kama zana ya ziada kwa wanawake walio katika "hatari kubwa ya VVU" na wadhibiti katika zaidi ya nchi kumi na mbili za Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Malawi, Uganda na Zimbabwe pia wametoa ruhusa.

WHO ilielezea tafiti mbili na uidhinishaji wake, ikisema kifaa hicho kilipunguza uwezekano wa wanawake kupata VVU kwa takribani theluthi moja, wakati utafiti mwingine umependekeza hatari inaweza kupunguzwa kwa zaidi ya asilimia 50.

Forum

XS
SM
MD
LG