Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:16

Wananchi Haiti wasubiri hatima ya Polisi wa Kenya

Jaji wa Mahakama ya Kenya Jaji Chacha Mwita akisikiliza ombi la kupinga kutumwa kwa vikosi vya Kenya kwenda Haiti, katika mahakama ya Milimani katika mji mkuu wa Nairobi, Kenya, Alhamisi, Novemba 16, 2023.

Watu kote nchini Haiti wanashangaa nini kitatokea  baada ya mahakama nchini Kenya kuzuia kupelekwa  kwa kikosi cha polisi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusaidia kupambana na magenge katika nchi hiyo ya Carribean  yenye matatizo.

Kutokuwa na uhakika na hofu vimekuwa vikitanda tangu uamuzi wa Ijumaa, huku ghasia zikifikia rekodi mpya wakati magenge yakiimarisha udhibiti wao katika mji mkuu wa Haiti na kwingineko. Rais wa Kenya William Ruto amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Haijulikani ni muda gani hiyo inaweza kuchukua na kama nchi nyingine ambazo ziliahidi kutuma vikosi vidogo ili kuimarisha operesheni ya mataifa mengi zingezingatia kufanya hivyo pekee. Miongoni mwa waliopanga kutuma vikosi ni Bahamas, Jamaica, Belize, Burundi, Chad na Senegal.

Forum

XS
SM
MD
LG