Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 15:36

Israeli yadai Hezbollah wameishambulia kwa kutumia zaidi ya roketi 30


Picha iliyopigwa karibu na mji wa Marjayoun kusini mwa Lebanon ikionyesha moja ya roketi zilizorushwa zikilenga Israeli.
Picha iliyopigwa karibu na mji wa Marjayoun kusini mwa Lebanon ikionyesha moja ya roketi zilizorushwa zikilenga Israeli.

Jeshi la Israel limesema kwamba takriban roketi 30 zimerushwa kaskazini mwa Israel usiku wa kuamkia leo, kutoka Lebanon kufuatia shambulizi la droni la Israel lililojeruhi kamanda wa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono la Iran, kusini mwa Lebanon.

Kwa mujibu wa shirika la habri la AFP, msemaji wa kijeshi wa Israel amesema kwamba wanaweza kudhibitisha kuwa takriban roketi 30 zimerushwa kutoka Lebanon kuelekea kwenye maeneo ya Ein Zeitim na Dalton kaskazini mwa Israel, likiongeza kuwa ripoti za awali zilisema kuwa hakuna watu waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo.

Jeshi la Israel limesema kwamba droni yake ilijeruhi kamanda wa Hezbollah kusini mwa Lebanon, likidai kuwa alihusika kwenya mashambulizi dhidi ya Israel.

Jeshi hilo liliongeza kusema kwamba mashambulizi ya Hezbollah yalilenga Kiryat Shmona na Metula, kaskazini mwa Israel.

Shirika la habari la serikali ya Lebanon liliripoti kuwa gari moja lilishika moto baada ya kugongwa na silaha iliyorushwa na droni ya Israel, lilipokuwa likiingia mjini.

Mkuu wa jeshi la wanahewa la Israel Tomer Bar ameonya kuwa iwapo mapigano yatazuka kwenye mpaka wa Lebano, basi kutakuwa na majibizano makali yakilenga mamia ya sehemu ndani ya Lebanon, ikiwemo miji ya Tyre, Sidon, Beirut na Bekaa.

Forum

XS
SM
MD
LG