Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:07

Shambulio lililomlenga mkuu wa ujasusi wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran limeuwa watu 12

Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran
Rais wa Iran Ebrahim Raisi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran

Shambulio lililomlenga mkuu wa ujasusi wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran huko Damascus na kulaumiwa Israel liliua watu 12, shirika linalofuatilia  vita lilisema Jumapili katika idadi iliyosahihishwa.

Shambulio lililomlenga mkuu wa ujasusi wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran huko Damascus na kulaumiwa Israel liliua watu 12, shirika linalofuatilia vita lilisema Jumapili katika idadi iliyosahihishwa.

Idadi ya vifo imeongezeka hadi 12 Wairani watano, ikiwa ni pamoja na viongozi watatu wa IRGC, Wasyria wanne wanaofanya kazi na Wairani, wawili wa Lebanon, na raia mmoja wa Iraq, lilisema Shirika la Syrian Observatory for Human Rights la Syria juu ya shambulio hilo la Jumamosi.

Shirika hilo la ufuatiliaji lenye makao yake nchini Uingereza na mtandao wa vyanzo ndani ya Syria hapo awali waliripoti vifo 10.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limethibitisha kuwa limepoteza askari watano katika shambulio ambalo liliilaumu Israel, adui wake mkuu wa eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG