Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:40

Kurdistan: Revolutionary Guards washambulia 'makao makuu ya ujasusi' ya Israel


Picha hii iliyopigwa na kutolewa Jan. 16, 2024, lna kituo cha 24 cha matangazo cha Kurdistan kinaonyesha wazimamoto na maafisa wa usalama katika eneo ambalo limeathiriwa na shambulizi la kombora lililopigwa na Iran, huko Irbil.
Picha hii iliyopigwa na kutolewa Jan. 16, 2024, lna kituo cha 24 cha matangazo cha Kurdistan kinaonyesha wazimamoto na maafisa wa usalama katika eneo ambalo limeathiriwa na shambulizi la kombora lililopigwa na Iran, huko Irbil.

Walinzi wa kikosi cha mapinduzi  Iran  maarufu  Revolutionary Guards walisema wameshambulia 'makao makuu ya ujasusi' ya Israel katika mkoa wa Kurdistan wenye utawala kiasi,  vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Jumatatu jioni.

Iran yakishambulia kikundi IS

Wakati huo huo kikosi hicho mahiri kilisema pia kimefanya shambulizi nchini Syria dhidi ya Islamic State.

Mashambulizi hayo yamekuja huku kukiwa na wasiwasi wa kuenea kwa mgogoro ambao umesambaa kote Mashariki ya Kati tangu vita kati ya Israel na kikundi cha Kiislam cha Palestina Hamas kuanza Oktoba 7, huku washirika wa Iran wakiingia katika mgogoro huo kutoka Lebanon, Syria, Iraq na Yemen.

“Katika kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni, yaliyosababisha mauaji ya makamanda wa kikosi cha Revolutionary Guards na mhimili wa upinzani … moja ya makao makuu muhimu ya ujasusi ya Mossad katika mkoa wa Kurdistan nchini Iraq kiliharibiwa na makombora ya masafa marefu,” Guards ilisema katika taarifa yake.

Maafisa wa Israeli

Maafisa wa serikali ya Israeli hawakuweza kupatikana mara moja kutoa maoni yao.

Zaidi ya mshambulizi hayo huko kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Kurdistan, Erbil katika eneo la makazi ya watu karibu na ubalozi mdogo wa Marekani, Guards walisema: “wamefyatua makombora ya masafa marefu kadhaa nchini Syria na kuwaangamiza wanaoendesha operesheni za kigaidi” nchini Iran, ikiwemo Islamic State.

Islamic State

Kikundi cha Islamic State kilidai kuhusika na milipuko miwili huko Iran mwezi huu ambayo iliuwa karibu watu 100 na kuwajeruhi wengine kadhaa katika kumbukumbu ya kamanda wa juu Qassem Soleimani.

“Tunalihakikishia taifa letu kuwa operesheni za mashambulizi za Revolutionary Guards zitaendelea na ulipizaji kisasi hadi tone la mwisho la damu la mashahidi wetu,” taarifa ya Guards ilisema.

Iran tayari iliahidi kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanajeshi wake watatu wa Republikan Guards nchini Syria mwezi uliopita, ikiwemo kamanda wa juu wa Guards, ambaye alihudumu kama washauri wa kijeshi huko.

Jeshi la Israel lakataa kutoa maelezo

Vyanzo vitatu vya usalama na chombo cha habari cha serikali ya Iran walisema wakati huo waliuawa katika shambulizi la anga la Israeli. Msemaji wa jeshi la Israel alikataa kutoka maoni yake, akisema ilikuwa ni kazi yake kulinda maslahi ya usalama ya Israel.

Iraq Yapinga Mashambulizi ya Iran

Wakati ikimwita balozi wake kutoka Tehran, Iraq ilimwita kaimu balozi wa Iran mjini Baghdad kupinga mashambulizi hayo, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Ilisema Baghdad itachukua hatua zote za kisheria dhidi ya kile ilichokiita ukiukaji wa uhuru wa Iraq.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imelaani mashambulizi hayo yaliyofanyika karibu na Erbil, wakiyaita ya “ovyo.” Lakini maafisa hao walisema hakuna ofisi za Marekani zilizokuwa zimelengwa na hapakuwa na vifo vya Wamarekani.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG