Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:12

Wakazi wa Ukanda wa Gaza waripoti mapigano makali kati ya majeshi ya Israeli na Hamas


Majeshi ya Israeli yakiendesha operesheni zao wakati vita vikali vikiendelea katika yao na wapiganaji wa Hamas huko Ukanda wa Gaza(Picha na Jeshi la Israeli / AFP) / )
Majeshi ya Israeli yakiendesha operesheni zao wakati vita vikali vikiendelea katika yao na wapiganaji wa Hamas huko Ukanda wa Gaza(Picha na Jeshi la Israeli / AFP) / )

Israel imefanya mashambulizi ya anga kote Ukanda wa Gaza Jumanne, huku wakazi wakiripoti mapigano makali kati ya majeshi ya Israeli na wanamgambo  wa Hamas katikati na kusini mwa Gaza.

Mapigano ya Jumanne yalihusisha eneo la Al-Bureij katikati ya eneo la Palestina na mji wa Khan Younis, ulioko kusini ambao ni wa pili kwa ukubwa huko Gaza.

Jeshi la Israeli pia limeripoti kufanya mashambulizi mapya huko kusini mwa Lebanon yakiwalenga wanamgambo wa Hezbollah, washirika wa Hamas ambao wamekuwa wakipambana na majeshi ya Israeli kuvuka mpaka wakati wote huu wa vita hivi vinavyoendelea huko Gaza.

Israel pia imeeleza imeshambulia miundombinu ya kijeshi inayomilikiwa na jeshi la Syria” kujibu kwa kile ilichosema ni mashambulizi kutoka eneo la Syria dhidi ya Israel.

(FILES) Rais wa Syria Bashar al-Assad (Picha ya Facebook.)
(FILES) Rais wa Syria Bashar al-Assad (Picha ya Facebook.)

Shirika la habari la serikali ya Syria lilisema mashambulizi kadhaa ya Israeli yalipiga nje ya Damascus na kusababisha “uharibifu wa vifaa.”

Israel imeonya kuwa, iwapo Hezbollah haitasitisha mashambulizi, vita kamili dhidi ya Lebanon vinaelekea kutokea. Wote Hamas na Hezbollah wanaungwa mkono na Iran, ambapo wanamgambo washirika wake nchini Syria, Iraq na Yemen wamekuwa wakifanya mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya Israel.

Israel imeashiria awamu mpya ya mashambulizi yake huko Ukanda wa Gaza kwa kutangaza Jumatatu itakuwa ikipunguza idadi ya wanajeshi wake huko Gaza wakati wakiendelea kulenga zaidi operesheni zake dhidi ya Hamas huko katika eneo la Gaza.

Vifaru vya Israel vikiwa vimejipanga huko katika mpaka kati yao na Ukanda wa Gaza Januari 2, 2024.(Photo by JACK GUEZ / AFP)
Vifaru vya Israel vikiwa vimejipanga huko katika mpaka kati yao na Ukanda wa Gaza Januari 2, 2024.(Photo by JACK GUEZ / AFP)

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi la Israel imesema kuondolewa kwa wanajeshi hao kunatarajiwa kupunguza mzigo mkubwa wa kiuchumi” na kuruhusu majeshi “kukusanya nguvu wakijiandaa na shughuli zijazo katika mwaka huu, wakati mapigano yataendelea, na huduma zao bado zitahitajika.”

Israel pia imeondoa vifaru vyake kutoka baadhi ya wilaya za Gaza, kulingana na wakazi walioko huko.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP, na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG