Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:29

Vifaru zaidi vya Israel vyaingia Gaza Jumapili


Vifaru vya Israel vikiingia Israel mwishoni mwa wiki
Vifaru vya Israel vikiingia Israel mwishoni mwa wiki

Vifaru vya Israel vimeingia ndani zaidi katikati na kusini mwa Gaza Jumapili, vikijisukuma katika kambi za wakimbizi za Bureij, Nuseirat na Maghazi pamoja na mji wa kusini wa Khan Younis, huku vikifanya mashambulizi. 

Mashambulizi makali ya anga yameuwa watu 165 na kujeruhi wengine 250 huko Gaza katika muda was aa 24 zilizopita, kwa mujibu wa mamlaka ya afya katika eneo linaloongozwa na Hamas. Huko Khan Younis, mji ulio karibu na mpaka wa Misri ambako maelfu ya wakimbizi wamekimbilia kutafuta hifadhi, waliojeruhiwa wako katika hospitali ya Nasser, moja ya kituo kikubwa sana cha afya upande wa kusini.

Jeshi la Israel limesema majengo mawili ya Hamas yamevunjwa huko Beit Lahia, kaskazini mwa Gaza. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema katika mkutano na wana habari jana Jumamosi kuwa eneo la mpakani kati ya Ukanda wa Gaza na Misri ni vyema liwe chini ya udhibiti wa Israel ili kuhakikisha kuwa eneo hilo halina silaha.

Netanyahu amesema kwamba ‘zaidi ya magaidi 8,000’ wameuawa hadi hivi sasa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza wakati taifa likijitayarisha kwa mapambano katika kila upande.’‘Vita vimeingia katika hatua kamili," Tunapigana kila upande. Tuna mafanikio makubwa, lakini pia tumepata maumivu.

Forum

XS
SM
MD
LG