Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:15

Wafanyakazi wa meli ya Ugiriki ilioshikiliwa na Iran waripotiwa kuwa salama


Meli ya St Nikolas ya Ugiriki iliyoshikiliwa na Iran baada ya kukamatwa ikiwa kwenye Ghuba ya Yemen.
Meli ya St Nikolas ya Ugiriki iliyoshikiliwa na Iran baada ya kukamatwa ikiwa kwenye Ghuba ya Yemen.

Wafanyakazi wa meli ya mizigo iliyoshikiliwa na Iran wiki iliyopita kutokana na mzozo na Marekani wapo salama, wamiliki wa meli hiyo kutoka Ugiriki wamesema Jumapili.

Kampuni ya Empire Navigation, inayoimiliki imesema kupitia taarifa kwamba mshirika wake amewasiliana na mamlaka za Iran, na kuripoti kwamba wafanyakazi wote waliokuwa kwenye meli hiyo kwa jina St Nikolas, wapo salama na wenye buheri ya afya.

Kampuni hiyo imeongeza kwamba haijaweza kuwasiliana moja kwa moja na wafanyakazi wote 19 wa meli hiyo iliyopeperusha bendera ya visiwa vya Marshall, na kulazimishwa na Iran kutia nanga kwenye bandari ya Bandar Abbas.

Miongoni mwa wafanyakazi hao,18 ni raia wa Ufilipino, na mmoja raia wa Ugiriki. Iran ilisema kwamba ilikamata meli hiyo karibu na Oman Alhamisi, kulalamikia wizi wa mafuta yake kutoka kwenye meli hiyo na Marekani mwaka jana, wakati huo ikijulikana kama Suez Rajan, chombo cha habari cha serikali kimesema.

Forum

XS
SM
MD
LG