Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 20:20

Blinken aonya baada ya wa-Houthi kuanzisha mashambulizi ya angani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken

“Mashambulizi haya yamesaidiwa na kuchochewa na Iran kwa teknolojia, vifaa, ujasusi, na yana athari ya kweli kwa  maisha ya watu” alisema Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken katika juhudi zake za hivi karibuni za kidiplomasia za kuzuia vita vya Gaza kusambaa, ameonya kuhusu “matokeo” baada ya waasi wa ki-Houthi wenye makao yake Yemen kuanzisha mashambulizi yao makubwa zaidi ya angani katika Bahari ya Sham.

“Tulikuwa na shambulio kubwa Zaidi, makombora ya UAVs - yasiyo na rubani, jana tu”, Blinken aliwaambia waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bahrain mjini Manama siku ya Jumatano.

“Mashambulizi haya yamesaidiwa na kuchochewa na Iran kwa teknolojia, vifaa, ujasusi, taarifa, na yana athari ya kweli kwa maisha ya watu”. Zaidi ya nchi 20, ikiwemo Bahrain zimeapa kulinda uhuru wa kusafiri na uhuru wa meli katika Bahari ya Sham, Blinken alisema baada ya kufanya mazungumzo na Mfalme wa Bahrain, Hamad bin Isa Al Khalifa.

Forum

XS
SM
MD
LG