Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 17:52

Antony Blinken azungumzia juhudi za kuwaachilia mateka wanaoshikiliwa na Hamas


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa kwenye kikao.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa kwenye kikao.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alizungumzia juhudi za kuwaachilia mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Gaza alipokutana Alhamisi na wajumbe wa baraza la mawaziri la vita la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Mwanzoni mwa mkutano wake na wakuu wa zamani wa kijeshi Benny Gantz na Gabi Eisenkot, Blinken alisema lengo litakuwa juu ya mateka na nia kubwa ambayo sisi sote tunayo ya kuwaona wakirudishwa kwenye familia zao, kazi inayofanywa ili kufikia lengo hilo.

Blinken pia alisema atatoa maelezo juu ya mikutano aliyofanya mahali pengine katika eneo hilo katika safari ambayo imejumuisha vituo vya Saudi Arabia, Misri, Qatar na Ukingo wa Magharibi

Gantz alimwambia Blinken kwamba suala la dharura zaidi ni kutafuta njia za kuwarudisha mateka.

Forum

XS
SM
MD
LG