Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:06

Blinken akutana na viongozi wa Misri na Qatar kushinikiza sitisho la mapigano Gaza


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo, Februari 6, 2024.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo, Februari 6, 2024.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumanne alikutana na viongozi wa Misri na Qatar huku kukiwa na msukumo kwa sitisho jipya la mapigano huko Gaza na kuongeza misaada ya kibinadamu kwa raia wa Palestina.

Mjini Cairo, Blinken alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi kabla ya kusafiri kuelekea Doha kukutana na kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, na waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani.

Marekani, Misri na Qatar zilisaidia kupatikana kwa pendekezo la sitisho la mapigano ambalo linafanyiwa kazi sasa, ambalo litajumuisha sitisho la muda la mapigano kwa kipindi cha wiki kadhaa na kuachiliwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.

“Kazi hivi sasa ipo upande wa Hamas,” Afisa mkuu katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliwaambia waandishi wa habari. Afisa huyo alisema Misri na Qatar ziliishinikiza Hamas kukubali kile Marekani ilichokielezea kama “pendekezo linalozingatia matakwa ya pande zote,” lakini Hamas inatakiwa hatimaye kulikubali.

Sitisho la mapigano la awali, mwishoni mwa mwezi Novemba lilidumu wiki moja na lilipelekea kuachiliwa huru kwa zaidi ya mateka 100 kutoka Gaza na wafungwa 240 wa Palestina waliokuwa wanashikiliwa na Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG