Baada ya wiki kadhaa ya juhudi za kidiplomasia, Misri, Qatar na Marekani zimekuwa zikihangaika kufanikisha mapendekezo ya wiki sita kusitisha vita kati ya Israel na Hamas kabla ya mwezi wa Ramadhani kuanza wiki ijayo.
Pendekezo hilo pia linajumuisha kuachiliwa watu waliochukuliwa wakati wa uvamizi wa Octoba 7 wa Hamas ambao umechochea vita kwa kubadilishana wafungwa wa Palestina wanaoshikiliwa na Israel.
Shirika la habari la Al- Qahera lenye uhusiano na idara ya kijajusi ya Misri imemnukuu afisa ambaye hakutajwa jina akisema kuwa “ Misri inaendelea na juhudi zake za kina kufikia makubaliano kabla ya mwezi wa Ramadhani waislamu wanafunga utakaoanza March 10 au 11.
“kumekuwa na maendeleo makubwa katika mashauriano hayo, taarifa hiyo imesema baada ya mazungumzo ya karibuni kuanza Jumapili mjini Cairo bila ya uwakilishi wa Israel.
Kwa mujibu wa afisa wa juu wa Marekani, Israel imekubali masharti ya makubaliano ya wiki sita ambayo yatasababisha kupelekwa msaada zaidi huko Gaza.
Forum