Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:51

Utawala wa kijeshi nchini Guinea wamteua waziri mkuu mpya


mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Guinea Mamady Doumbouya (katikati) akiwa na wajumbe wa ECOWAS Septemba 5 2021. Picha na JOHN WESSELS / AFP
mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Guinea Mamady Doumbouya (katikati) akiwa na wajumbe wa ECOWAS Septemba 5 2021. Picha na JOHN WESSELS / AFP

Utawala wa kijeshi nchini Guinea Jumanne ulisema umemteua waziri mkuu mpya siku nane baada ya kuivunja serikali ya awali, huku shughuli katika mji mkuu wa Conakry zikizorota kwa siku ya pili ya mgomo wa kitaifa.

Waandamanaji wanaomba kiongozi wa chama cha wafanyakazi anayezuiliwa aachiliwe na kupunguza pia bei ya chakula, kukomesha udhibiti wa vyombo vya habari na kuboresha hali ya maisha kwa wafanyakazi wa serikali.

Mgomo huo uliitishwa katika hali ya ongezeko la mvutano wa kijamii na kutokuwepo kwa serikali ya mpito baada ya utawala wa kijeshi kutangaza kuvunjwa kwa serikali wiki iliyopita, bila kueleza sababu.

Katika hotuba kwenye televisheni ya taifa Jumanne jioni, msemaji wa kiongozi wa utawala wa kijeshi Jenerali Mamady Doumbouya alisema “ Bwana Amadou Oury Bah, mchumi, anateuliwa kuwa waziri mkuu na kiongozi wa serikali.”

Msemaji huyo alisema jukumu kubwa la Oury Bah itakuwa kupunguza mvutano na vyama 13 vya wafanyakazi ambavyo viliitisha mgomo ulioanza siku ya Jumatatu, ambao ulisababisha vifo vya watu wawili waliopigwa risasi wakati wa vurugu katika vitongoji vya mji wa Conakry.

Shule, maduka, masoko na barabara zilikuwa tena tupu Jumanne na hospitali zilitoa tu huduma za dharura.

Forum

XS
SM
MD
LG