Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:34

Rais wa Nigeria aagiza maafisa wa usalama kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara bila kulipa fidia


Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu

Rais wa Nigeria aliamuru maafisa wa usalama kutolipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi waliotekwa nyara na watu wenye silaha wiki iliyopita, waziri wa habari alisema Jumatano.

Ndugu wa wanafunzi hao wanasema watekaji nyara wameomba fidia kubwa ili kuwaachilia wanafunzi waliotekwa nyara shuleni mwao Alhamisi iliyopita katika kijiji cha Kuriga kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna.

Magenge ya wahalifu mara nyingi huteka nyara watu wengi kaskazini mwa Nigeria, yakilenga shule, vijiji na barabara kuu.

Katika miaka mitatu iliyopita, mamia ya wanafunzi walitekwa nyara. Waathirika wa utekaji nyara nchini Nigeria mara nyingi huachiwa huru baada ya mazungumzo na mamlaka, ingawa maafisa wanakanusha malipo ya fidia kufanyika.

Kwa kuzingatia msimamo rasmi wa serikali, waziri Mohammed Idris alisema Rais Bola Tinubu aliwaambia maafisa wa usalama wanaowatafuta wanafunzi kuhakikisha “hakuna hata senti moja inayolipwa”.

“Rais ameviagiza vyombo vya usalama kwamba kwa sababu ni suala la dharura lazima vihakikishe watoto hawa na wale wote waliotekwa nyara wanarejeshwa nyumbani wakiwa salama,” aliwambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri katika mji mkuu Abuja.

CN: AP

Forum

XS
SM
MD
LG