Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wameanzisha mchakato wa kuomba msaada wa ufadhili wa fedha ili kukabiliana na athari mbaya za mvua kubwa zinazonyesha kwa miezi kadhaa ambazo zimewakosesha makazi takriban watu 100,000.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi hasimu cha wanamgambo yaliua raia 25 katika mji wa kaskazini mwa Darfur wa El-Fasher, kundi la wanasheria wanaotetea demokrasia lilisema Jumanne.
Wataalam wa kijeshi wa Russia wamewasili Niger wakiwa wamebeba mfumo wa ulinzi wa anga pamoja na vifaa vingine kama sehemu ya taifa hilo la Afrika Magharibi kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na Moscow, televisheni ya serikali imesema Alhamisi.
Umoja wa Ulaya umesema Ijumaa kuwa utaipatia Misri dola bilioni 1.7 kama msaada wa muda mfupi ili kuisaidia nchi hiyo kujenga uchumi wake.
Polisi nchini Ethiopia wamewakamata washukiwa 13 juu ya mauwaji ya kiongozi maarufu wa upinzani kutoka jimbo la Oromia, chombo cha habari cha ndani kimesema.
Ukraine ilifungua ubalozi wake Alhamisi nchini Ivory Coast, siku moja baada ya kufungua ubalozi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku Kyiv ikitafuta uwepo wake zaidi barani Afrika kukabiliana na ushawishi wa Russia.
Takriban watu milioni 3.4 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Chad kufuatia kuwasili kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan wanaoikimbia vita, shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa lilionya Jumatano.
Utawala wa kijeshi nchini Mali Jumatano uliamuru kusimamishwa kwa shughuli zote za vyama vya siasa, ukisema hatua hiyo inahitajika ili kudumisha usalama wa umma.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Jumanne alimuagiza waziri wake mkuu kuandaa “mpango wa dharura” wa kuimarisha uchumi na sekta ya fedha iliyo katika hali ngumu nchini humo, ofisi yake ilisema katika taarifa.
Togo imepanga tena kuwa uchaguzi wa bunge utafanyika tarehe 29 Aprili baada ya kuuahirisha kutokana na mageuzi ya katiba yenye utata, taarifa ya serikali ilisema Jumanne.
Mahakama ya Afrika Kusini Jumanne iliamua kwamba rais wa zamani Jacob Zuma anaweza kugombea kwenye uchaguzi mkuu, na hivyo kubatilisha uamuzi uliochukuliwa na tume ya uchaguzi kumkatalia kuwania kufuatia kesi iliyompata na hatia.
Majaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa zamani Jacob Zuma ataruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi wa Mei.
Shambulio la kombora mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo liliua wanajeshi watatu wa Tanzania ambao walikuwa katika kikosi cha SADC kilochopelekwa huko kusaidia wanajeshi wa serikali ya DRC kupambana na waasi wa M23, maafisa walisema.
Taifa la Nicaragua Jumatatu Limetoa wito kwa Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa kusitisha misaada wa kijeshi ya Ujerumani na misaada mingine kwa Israel.
Watu 20 waliuawa Jumapili katika mapigano katika mkoa wa Syria wa Daraa siku moja baada ya mlipuko kuua kundi la watoto, shirika la haki za binadamu linalofuatilia vita limesema.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumapili alisema kwamba Ukraine itashindwa katika vita vyake dhidi ya Russia ikiwa Bunge la Marekani halitaidhinisha msaada mkubwa wa kijeshi, huku wanajeshi wa Russia wakiendelea kujiimarisha kwenye uwanja wa mapambano.
Zaidi ya watu 90 walifariki wakati boti iliyojaa watu wengi ilipozama katika pwani ya kaskazini mwa Msumbiji, mamlaka za eneo hilo zilisema Jumapili.
Maktaba ya Taifa ya Haiti imevunjwa na magenge yenye silaha yanayowatisha watu katika mji mji mkuu wa Port-au-Prince kwenye taifa hilo la Carribean, mkurugenzi wa maktaba hiyo ameiambia AFP, ambapo UNESCO imelaani mashambulizi kadhaa ya uharibifu katika taasisi za Elimu na Sanaa nchini humo.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Guangzhou leo Alhamisi kuanzia ziara ya ufuatiliaji huko China ikiwa ni chini yam waka mmoja.
Pandisha zaidi