Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:16

Watu 20 wauawa katika mapigano nchini Syria


Ramani ya Syria
Ramani ya Syria

Watu 20 waliuawa Jumapili katika mapigano katika mkoa wa Syria wa Daraa siku moja baada ya mlipuko kuua kundi la watoto, shirika la haki za binadamu linalofuatilia vita limesema.

Daara ulikuwa mkoa ambapo uasi dhidi ya Rais Bashar al-Assad uliibuka mwaka 2011, lakini ulirejea chini ya udhibiti wa serikali mwaka 2018 kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoungwa mkono na Russia.

Mkoa huo wa kusini mwa nchi umekumbwa na mzozo tangu wakati huo.

The Syrian Observatory for Human Rights lilisema Ahmed al-Labbad, ambaye “anaongoza kundi la waasi,” ameshtumiwa na kundi hasimu kwa kutega bomu ambalo liliua watoto wanane Jumamosi katika mji wa Al-Sanamayn.

Labbad, ambaye awali alifanya kazi kwenye idara ya usalama ya serikali, alikanusha kuhusika na mauaji hayo, shirika hilo linalofuatilia vita lenye makao yake Uingereza lilisema.

Jumapili, kundi hasimu la waasi linaloongozwa na mtu ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa kundi la Islamic State na akiwa hivi sasa mshirika wa idara ya ujasusi ya jeshi, aliingia katika mji wa Sanamayn na mapigano yakazuka, shirika hilo limesema.

Washambuliaji walichoma nyumba za familia ya Labbad na kuwaua wanaoishi ndani ya nyumba hizo, shirika hilo liliongeza.

Miongoni mwa watu 20 waliouawa, watatu walikuwa kutoka familia ya Labbad na 14 walikuwa wapiganaji wake, shirika hilo limesema.

Vyombo vya habari vya serikali ya Syria havikuripoti mara moja mapigano hayo. Shirika la habari la serikali SANA limenuku polisi wakisema watoto saba waliuawa katika mlipuko wa Jumamosi katika mji wa Sanamayn, wakiwashtumu “magaidi” kuhusika na shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG