Mkurugenzi wa Maktaba Dangelo Neard alisema kuwa historia ya Haiti – Ukanda wa Magharibi wa jamhuri ya pili kongwe – ilikuwa inatishiwa usalama wake.
“Mkusanyiko wa nyaraka zetu ziko hatarini. Tuna nyaraka ambazo ni nadra kupatikana za zaidi ya miaka 200, zenye umuhimu na turathi zetu, ambazo ziko hatarini kuchomwa moto au kuharibiwa na majambazi,” alisema.
“Niliambiwa kuwa wahuni hawa wanachukua samani za taasisi zetu. Pia wameiba jenereta la jengo hilo.”
Makundi yenye silaha yanadhibiti sehemu kubwa ya Port-au-Prince na maeneo ya pembeni mwa nchi kutokana na kukosekana kwa serikali inayofanya kazi na kuendelea kuchelewa kuundwa mamlaka ya mpito iliyoahidiwa.
Baada ya siku kadhaa za utulivu kiasi, mashambulizi yalirudi tena katika maeneo kadhaa ya jirani ya Port-au-Prince kuanzia Jumatatu.
Shambulizi hilo katika Maktaba ya Taifa limekuja baada ya mashambulizi kadhaa wiki iliyopita katika vyuo vikuu viwili, Ecole Normale Superieure na National School of Arts.
Forum