Boti hiyo iliyokuwa ya uvuvi ilikuwa imebeba watu 130, ilipata matatizo ilipojaribu kufika kwenye kisiwa kilicho karibu na mkoa wa Nampula, maafisa walisema.
“Kwa sababu boti hiyo ilikuwa imejaa watu wengi na haikufaa kubeba abiria iliishia kuzama. Kuna watu 91 waliofariki,” alisema katibu wa mkoa wa Nampula Jaime Neto.
Aliongeza kuwa watoto wengi ni miongoni mwa waliokufa.
Waokoaji walipata manusura watano na walikuwa wakiwatafuta wengine zaidi, lakini hali mbaya ya hewa baharini ilifanya operesheni ya kuokoa watu kuwa ngumu.
Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika, moja ya nchi maskini zaidi duniani, imerekodi takriban visa 15,000 vya ugonjwa unaosababishwa na maji machafu na vifo 32 tangu mwezi Oktoba, kulingana na takwimu za serikali.
Mkoa wa Nampula ndilo eneo lililoathiriwa zaidi, ukiwa na theluthi moja ya visa vyote.
Forum