Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 23:43

Watu milioni 3.4 wakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Chad


Wakimbizi wa Sudan waliokimbilia Chad wakipiga foleni kuchota maji katika kambi ya wakimbizi ya Adre, Disemba 7, 2023. Picha ya AFP
Wakimbizi wa Sudan waliokimbilia Chad wakipiga foleni kuchota maji katika kambi ya wakimbizi ya Adre, Disemba 7, 2023. Picha ya AFP

Takriban watu milioni 3.4 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Chad kufuatia kuwasili kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan wanaoikimbia vita, shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa lilionya Jumatano.

“Mikoa ya mashariki mwa Chad ni miongoni mwa maeneo yaliyo hatarini yakiwa na huduma mbovu za msingi, na kuwasili kwa wakimbizi kumezidisha sana mahitaji, shirika la Action Against Hunger lilisema katika taarifa.

Umoja wa mataifa ulionya mwezi Machi kwamba msaada wa chakula cha kuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaoingia kwa wingi kutoka nchi ya Sudan inayokumbwa na vita, utamalizika mwezi Aprili ikiwa hakuna ufadhili wa kimataifa.

Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) liliomba msaada wa dola milioni 242 kuepuka janga na kuendelea kusaidia wakimbizi wa Sudan milioni 1.2, huku msimu wa mvua unaokaribia ukitishia kukata barabara ya kusafirisha msaada wa kibinadamu mashariki mwa Chad.

Nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati tayari ilikuwa moja ya nchi maskini duniani, huku watu milioni 1.4 wakiwa wakimbizi wa ndani au kutoka nchi jirani.

Forum

XS
SM
MD
LG