Waandamanaji wanaoipinga serikali wanakusanyika nje ya Bunge la Israel mjini Jerusalem na kuandamana hadi kwenye makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wakitaka uchaguzi wa mapema na makubaliano ya kutekwa nyara huku kukiwa na hasira juu ya jinsi vita vya Gaza vilivyoshughulikiwa.
Shambulio la ndege isiyokuwa na rubani liliua watu 12 na kujeruhi wengine 30 Jumanne katika mji wa kaskazini mashariki mwa Sudan wa Atbara, ambao kufikia sasa, ulikuwa umeepuka vita vya kikatili, madaktari na mashahidi wameliliambia shirika la habari la AFP.
Waziri wa mipango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka Jumatatu amekuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke katika taifa hilo la Afrika ya kati, televisheni ya serikali imetangaza.
Maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Afrika Kusini Alhamisi walisema kwamba wamemuondoa rais wa zamani Jacob Zuma kwenye kiny’anganyiro cha uchaguzi wa mwezi Mei, na hivyo kuzua mvutano katika maandalizi ya uchaguzi huo.
Basi moja nchini Afrika Kusini, Alhamisi ilitumbukia chini ya mlima kutoka kwenye daraja na kuwaka moto, na kuua watu 45 kati ya 46 waliokuwa ndani ya basi hilo, wizara ya uchukuzi ilisema.
Mivutano ya kisiasa imeongezeka nchini Togo tangu siku ya Jumatatno wakati polisi walipovunja mkutano na wanahabari uliyoitishwa na upinzani ikiwa ni kujibu mageuzi ya kikatiba ambayo yamekosolewa kuwa ni kujitwalia madaraka.
Rais wa Russia Vladimir Putin amewaonya washirika wa Ukraine, mataifa ya Magharibi, dhidi ya kutoa msaada wa vituo vya anga katika nchi zao.
Mahakama ya Iran ilimuhukumu kifo mkuu wa polisi kaskazini mwa Iran baada ya kushtakiwa kwa kumua mtu wakati wa maandamano makubwa mwaka 2022, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumatano.
Wagombea 10, wakiwemo wapinzani wawili wakali wa utawala wa kijeshi wa Chad, Jumatano waliandamana baada ya kuzuiliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa rais wa tarehe 6 Mei.
Utawala wa kijeshi nchini Mali ulipiga marufuku shughuli za muungano nadra wa vyama vya upinzani mjini Bamako ukitaja “vitisho vya kuvuruga usalama wa umma,” kulingana na amri rasmi ambayo AFP iliiona.
Zambia Jumatatu ilitangaza kwamba imeingia makubaliano ya kihistoria na wakopeshaji binafsi wanaomiliki Eurobond zenye thamani ya dola bilioni 3.5, na kuondoa kikwazo kikubwa katika marekebisho ya muda mrefu ya deni la nchi hiyo.
China ilisema Jumatatu inaunga mkono rasimu ya azimio jipya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu sitisho la “haraka" la mapigano huko Gaza, baada ya taifa hilo na Russia kupinga azimio la awali lililopendekezwa na Marekani.
Watu wanne wanaoshtumiwa kuhusika katika shambulio kwenye jumba la tamasha mjini Moscow ambalo liliua watu 137 Jumapili wameshtakiwa kwa makosa ya ugaidi na kuamriwa kuwekwa kizuizini kwa kusubiri kesi.
Watu 11 waliuawa katika mashambulizi mawili karibu na mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa eneo hilo waliiambia AFP Jumapili, wakituhumu kundi la waasi wa ADF kufanya mashambulizi hayo.
Zaidi ya watoto wa shule 130 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria mapema mwezi huu waliachiliwa Jumapili bila kujeruhiwa, maafisa na jeshi walisema.
Watazamaji wa televisheni kote duniani watapata ripoti maalum ya hali ya hewa Alhamisi wakati watoto watakapokuwa kwenye televisheni wakitoa utabiri maalum wa hali ya hewa kuhusu mustakabali wao – tishio la mgogoro wa hali ya hewa.
Milio ya risasi ilisikika huko Port-au-Prince baada ya siku tatu za utulivu wa kiasi, wakati ambapo mazungumzo ya kuundwa kwa mamlaka ya mpito yanaendelea kujaribu kuiondoa nchi hiyo ya Caribbean kutoka katika mgogoro wake mkubwa wa kisiasa .
Raia wa Russia walianza kupiga kura leo Ijumaa katika uchaguzi wa rais wa siku tatu unaotarajiwa kumkabidhi kiongozi mwenye msimamo mkali Vladimir Putin muhula mwingine wa miaka sita huku mashambulizi mapya yakiendelea nchini Ukraine hadi katika eneo la Russia.
Wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al-Shabab Alhamisi walishambulia hoteli maarufu karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi walisema.
Pandisha zaidi