Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:45

Zuma akataliwa kugombea urais


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Afrika Kusini Alhamisi walisema kwamba wamemuondoa rais wa zamani Jacob Zuma kwenye kiny’anganyiro cha uchaguzi wa mwezi Mei, na hivyo kuzua mvutano katika maandalizi ya uchaguzi huo.

Nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu tarehe 29 Mei, uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Chama tawala cha African National Congress(ANC) kiko katika hatari ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani mwishoni mwa enzi ya utawala wa ubaguzi.

Chama kinazidi kupoteza wafuasi kutokana na uchumi dhaifu na madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.

Zuma, mwenye umri wa miaka 81, alilazimika kuondoka madarakani mwaka wa 2018 chini ya wingu la madai ya ufisadi lakini bado ana umaarufu wa kisiasa.

Amekuwa akipiga kampeni kwa niaba ya chama cha upinzani cha uMkonto we Sizwe (MK) katika jaribio la kufufua tena hadhi yake, akiwaita wanachama wa chama chake cha zamani cha ANC, “wasaliti”.

“Kuhusu kesi ya rais wa zamani Zuma, ni kweli, tulipokea pingamizi, ambayo imekubaliwa,” mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Mosotho Moepya aliwaambia waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi.

Anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kabla ya tarehe 2 Aprili.

Forum

XS
SM
MD
LG