Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 22:37

Mali: Shughuli za muungano wa vyama vya upinzani zapigwa marufuku katika mji mkuu


Umati wa watu ukihudhuria ibada ya sala inayoongozwa na Imamu Mahmoud Dicko, mmoja wa viongozi wa upinzani, Agosti 28, 2020.
Umati wa watu ukihudhuria ibada ya sala inayoongozwa na Imamu Mahmoud Dicko, mmoja wa viongozi wa upinzani, Agosti 28, 2020.

Utawala wa kijeshi nchini Mali ulipiga marufuku shughuli za muungano nadra wa vyama vya upinzani mjini Bamako ukitaja “vitisho vya kuvuruga usalama wa umma,” kulingana na amri rasmi ambayo AFP iliiona.

Nchi hiyo imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mfululizo mwaka 2020 na 2021, huku hali ya usalama ikiambatana na mzozo wa kisiasa na kibinadamu.

Muungano huo uliopewa jina la “Action Synergy for Mali”, ulianzishwa mwezi Februari na unaundwa na vyama 30 vya upinzani wakiwemo wafuasi wa Imamu mwenye ushawishi mkubwa, Mahamoud Dicko.

“Kutokana na hali ya usalama na hatari ya vitisho kwa usalama wa umma,” shughuli za kundi la Action Synergy for Mali zimepigwa marufuku rasmi katika wilaya nzima ya Bamako,” ilisema amri hiyo iliyosainiwa Jumatatu na gavana wa Bamako Abdoulaye Coulibaly.

Muungano huo umetupilia mbali marufuku hiyo, ukiielezea kuwa “uamuzi usio halali unaokiuka uhuru wa kufanya mikutano na kujieleza unaokubaliwa na katiba”.

Kundi hilo ni mkosoaji mkubwa wa utawala wa kijeshi na lilipendekeza “njia mpya” kwa wanainchi wa Mali ambao wameshuhudia nchi yao ikiharibiwa na makundi tofauti yenye uhusiano na al-Qaeda na Islamic State tangu 2012.

Forum

XS
SM
MD
LG