Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:17

Ajali ya basi yaua watu 45 nchini Afrika Kusini


Ramani ya Afrika Kusini
Ramani ya Afrika Kusini

Basi moja nchini Afrika Kusini, Alhamisi ilitumbukia chini ya mlima kutoka kwenye daraja na kuwaka moto, na kuua watu 45 kati ya 46 waliokuwa ndani ya basi hilo, wizara ya uchukuzi ilisema.

Mtoto wa miaka minane ndiye manusura pekee na alipekwa hospitali akiwa na majeraha mabaya.

Gari hilo lilikuwa linaelekea Moria kaskazini mwa nchi likitokea nchi jirani ya Botswana, wizara hiyo ilisema katika taarifa.

“Inadaiwa kuwa dereva alishindwa kudhibiti gari na hivyo kugongana na vizuizi vya daraja na kusababisha basi hilo kupita juu ya daraja na kufika chini ambapo iliwaka moto,” taarifa hiyo ilisema.

Operesheni za uokoaji ziliendelea hadi nyakati za jioni huku baadhi ya miili ikiwa imechomeka sana kiasi cha kutotambulika, na wengine wakiwa wamekwama ndani ya mabaki au kusambaratika kwenye eneo la ajali.

Basi hilo ilikuwa na nambari ya leseni ya Botswana, maafisa wa eneo hilo walisema, lakini uraia wa abiria ulikuwa bado unakaguliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG