Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:26

Wanamgambo wa al-Shabab washambulia hoteli maarufu karibu na Ikulu


Picha hii inaonyesha hoteli maarufu ya SYL iliyoshambuliwa na wanamgambo wa al-Shabab mjini Mogadishu. Picha ya AP
Picha hii inaonyesha hoteli maarufu ya SYL iliyoshambuliwa na wanamgambo wa al-Shabab mjini Mogadishu. Picha ya AP

Wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al-Shabab Alhamisi walishambulia hoteli maarufu karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi walisema.

Shambulio hilo ambalo al-Shabab ilidai kuhusika, lilianza nyakati za saa tatu na dakika 45 usiku, wakati watu wenye silaha walipovamia hoteli ya SYL kwa risasi nyingi.

“Watu wengi wenye silaha waliingia kwa nguvu ndani ya jengo hilo baada ya kuharibu ukuta wa pembeni kwa mlipuko mkubwa,” afisa wa usalama Ahmed Dahir aliiambia AFP.

Haikufahamika mara moja ikiwa kuna vifo vilitokea.

Mashahidi walielezea kusikia washambuliaji wakifyatua risasi hovyo.

“Sina taarifa kuhusu majeruhi lakini kulikuwa na watu wengi ndani wakati shambulio hilo lilipoanza,” alisema Hassan Nur ambaye alitoroka kwa kupanda ukuta.

Forum

XS
SM
MD
LG