Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:57

Wagombea 10 wa urais nchini Chad waandamana baada ya fomu zao kupingwa


Wagombea wa urais kutoka muungano wa upinzani wakiwasilisha fomu zao kwenye Mahakama ya Katiba mjini N'Djamena, Machi 14, 2024. Picha ya AFP
Wagombea wa urais kutoka muungano wa upinzani wakiwasilisha fomu zao kwenye Mahakama ya Katiba mjini N'Djamena, Machi 14, 2024. Picha ya AFP

Wagombea 10, wakiwemo wapinzani wawili wakali wa utawala wa kijeshi wa Chad, Jumatano waliandamana baada ya kuzuiliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa rais wa tarehe 6 Mei.

Mahakama ya Katiba mjini N’Djamena Jumapili ilisema fomu zao zimepingwa kutokana na “kasoro”.

Waliapa katika mkutano na waandishi wa habari kwamba “watapinga” uamuzi huo na kufunga barabara na kusema utawala wa kifamilia wa Deby ni wa “udikteta”.

Wakipinga kile walichoita “maelezo ya kipuuzi ya mahakama”, mmoja kati ya wagombea hao 10 alisoma taarifa waliyosaini wote ambayo inaomba wanainchi kusimama kidete, na kutumia njia zote za kisheria “kuikoa nchi dhidi ya udikteta”.

Wito huo unatolewa mwezi mmoja baada ya mpinzani mkuu wa kiongozi wa Chad Jenerali Mahmat Idriss Deby Itno, Yaya Dillo kuuawa kwa risasi katika shambulio la jeshi dhidi ya makao makuu ya chama chake cha PSF.

Forum

XS
SM
MD
LG