Bunge la taifa hilo la Afrika Magharibi lilipiga kura kwa ajili ya katiba mpya siku ya Jumatatu, na kuabdili kutoka mfumo wa urais na kuingia katika mfumo wa bunge.
Huku ikiwa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa bunge, wapinzani wanakhofia kuwa hatua hiyo itafungua njia kwa Rais wa muda mrefu Faure Gnassingbe kubaki madarakani kwa mudo usio julikana.
Kiasi cha askari 30 waliojihami kwa silaha waliingilia kati mkutano huo, ambao uliitishwa na vyama vya upinzani na makundi ya kiraia kuzungumzia mabadiliko.
Maafisa wamesema tukio hilo kwenye makao makuu ya chama cha upinzani cha ADDI katika mji mkuu wa Lome halikupata idhini inayostahili, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa AFP aliyekuwa katika eneo.
Baadaye, mkuu wa chama cha upinzani cha National Alliance for Change – ANC, Jean Pierre Fabre alibeza mageuzi hayo katika mkutano mwingine na wanahabari.
Forum