Rais atachaguliwa bila mjadala na wabunge kwa muhula mmoja wa miaka sita", na sio na umma, kulingana na Katiba mapya.
Mabadiliko hayo yamefanyika chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi ujao wa wabunge, lakini bado haijajulikana ni lini mabadiliko hayo -- ambayo yalipitishwa kwa kura 89 za ndio, moja ya kupinga na moja kutopiga kura -- yataanza kutumika.
Hivi sasa, rais anaweza kuhudumu hadi mihula miwili ya miaka mitano, Mabadiliko ya katiba, yalipendekezwa na kundi la wabunge wengi wao kutoka chama tawala cha Union for the Republic (UNIR), yalipitishwa kwa karibu kwa kauli moja.
Upinzani nchini humo, ambao ulisusia uchaguzi uliopita wa wabunge mwaka wa 2018 na kushutumu "upungufu" katika zoezi la sensa ya wapiga kura, hauwakilishwi vyema katika bunge la kitaifa.
Katiba mpya pia inabuni nafasi ya mkuu wa baraza la mawaziri mwenye “mamlaka kamili ya kusimamia mambo ya serikali na kuwajibika ipasavyo.
Forum