Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 07:01

Washukiwa wanne wa shambulio la mjini Moscow washtakiwa kwa makosa ya ugaidi


Moto mkubwa waonekana juu ya jumba la tamasha mjini Moscow, Crocus City Hall, lililoshambuliwa na watu wenye silaha, Machi 22, 2024. Picha ya AP
Moto mkubwa waonekana juu ya jumba la tamasha mjini Moscow, Crocus City Hall, lililoshambuliwa na watu wenye silaha, Machi 22, 2024. Picha ya AP

Watu wanne wanaoshtumiwa kuhusika katika shambulio kwenye jumba la tamasha mjini Moscow ambalo liliua watu 137 Jumapili wameshtakiwa kwa makosa ya ugaidi na kuamriwa kuwekwa kizuizini kwa kusubiri kesi.

Wote wanne wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela, taarifa ya mahakama ya wilaya ya Basmanny mjini Moscow ilisema.

Watu hao waliamriwa kuzuiliwa hadi Mei 22, lakini muda huo unaweza kuongezwa kulingana na tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yao itakapopangwa.

Mahakama ilisema wawili kati ya washtakiwa walikiri hatia, mmoja wao kutoka Tajikistan, “alikubali kabisa hatia yake”, taarifa ya mahakama ilisema. Maafisa tayari walisema kuwa watu hao wenye silaha ni raia wa kigeni. Maafisa wa Russia walisema walikamata watu 11 kuhusiana na shambulio la Ijumaa usiku kwenye jumba la Crocus City katika kitongoji cha kaskazini mwa Moscow cha Krasnogorsk, wakiwemo wanne waliotekeleza mauaji hayo.

Licha ya kuwa kundi la Islamic State lilikiri kuhusika na shambulio hilo, Rais wa Russia Vladimir Putin ameonekana kudai kwamba Kyiv ilihusika aliposema Jumamosi kwamba watu hao walikamatwa wakijaribu kukimbilia nchini Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na Marekani walitupilia mbali madai yoyote kwamba Kyiv ilihusika.

Forum

XS
SM
MD
LG