Serikali ya kijeshi ya Niger Januari ilikubali kuongeza ushirikiano wake wa usalama na Russia baada ya kuvifukuza vikosi vya Ufaransa, vilivyokuwa vikikabiliana na wanajihadi kwenye mataifa kadhaa ya Sahel. Mapema Ijumaa. kikosi cha Russia cha African Corps ambacho kinaonekana kama mbadala wa kundi la mamluki la Wagner la Afrika kimethibitisha kuwasili Niger.
Televisheni ya Tele Sahel imeonyesha ndege ya mizigo ya Russia ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Niamey wiki hii. Mtaalam mmoja kutoka jeshi la Russia alinukuliwa akisema,” Tuko hapa kutoa mafunzo kwa jeshi la Niger na kulisaidia kutumia vifaa ambavyo tumeleta.
Niger moja wapo ya nchi masikini ulimwenguni imekuwa ikishirikiana na mataifa ya magharibi katika kukabiliana na wanajihadi kwenye eneo la Sahel, lakini sasa inaonekana kuigeukia Russia, tangu kuondolewa madarakani kwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Julai mwaka uliopita.
Forum