Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:50

Marekani inatathmini mustakbali wa operesheni zake eneo la Sahel


Jenerali Michael Langley, mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani katika kamandi ya Afrika. July 21, 2022.
Jenerali Michael Langley, mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani katika kamandi ya Afrika. July 21, 2022.

Jeshi la Marekani lina mamia ya wanajeshi walioko huko katika  kambi kubwa  ya jeshi la anga kaskazini mwa Niger

Marekani imeshughulika siku ya Jumapili kutathmini mustakabali wa operesheni zake za kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel baada ya utawala wa kijeshi wa Niger kusema inafuta ushirikiano wake wa kijeshi wa miaka mingi na Marekani kufuatia ziara ya maafisa wa juu wa Marekani.

Jeshi la Marekani lina mamia ya wanajeshi walioko huko katika kambi kubwa ya jeshi la anga kaskazini mwa Niger ambayo inapeleka ndege katika eneo kubwa la Sahel, kusini mwa jangwa la Sahara, ambako makundi ya jihadi yenye uhusiano na al-Qaeda na kundi la Islamic State yanaendesha shughuli zao.

Molly Phee, mjumbe wa ngazi ya juu Marekani
Molly Phee, mjumbe wa ngazi ya juu Marekani

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Marekani Molly Phee alirejea katika mji mkuu wa Niamey wiki hii kukutana na maafisa waandamizi wa serikali, akiandamana na Jenerali Michael Langley, mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani katika kamandi ya Afrika. Awali alitembelea huko mwezi Disemba, wakati kaimu naibu waziri wa mambo ya nje, Victoria Nuland aliposafiri kwenda nchini humo mwezi Agosti.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Jumapili katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, zamani ukiitwa Twitter, kwamba mazungumzo yalikuwa ya wazi na kwamba walikuwa wanawasiliana na utawala wa kijeshi. Haijabainika wazi iwapo Marekani inafanya njia yoyote ya mazungumzo katika makubaliano ya kuendelea kubaki nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG