Makundi ya kutetea haki yamesema katika ripoti zilizochapishwa wiki hii, kwamba matukio hayo yalitokea katika kipindi kati ya mwezi Desemba na Machi mwaka huu.
Mali pomoja na jirani zake Burkina Faso na Niger, kwa zaidi ya muongo mmoja zimekuwa zikipambana na uasi unaofanywa na makundi ya waislamu wenye itikadi kali, wakiwemo baadhi ya washirika wa al-Qaida na wa kundi la Islamic State .
Kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika mataifa yote matatu katika miaka ya hivi karibuni, uongozi wa kijeshi umekifukuza kikosi cha Ufaransa na badala yake kukigeukia kikosi cha mamluki wa Russia kwa msaada.
Ghasia zimeongezeka Mali tangu mamluki wa Russia walipowalisi kufuatia mapinduzi ya 2021. Uongozi wa kijeshi nchini humo umeanzisha oparesheni kali za ndege zisizo na rubani, mashambulizi ambayo yamelenga mkusanyiko wa watu na uvamizi uliosindikizwa na mamluki wa Russia ambao umeua watu.
Wakazi wa kanda ya Sahel ambayo inaijumuisha Mali wamesema kuwepo kwa Russia hakujaleta mabadiliko, hasa tangu kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin alipofariki katika ajali ya ndege inayotiliwa shaka.
Kwa mfano, Huma Rights inasema katika uvamizi uliofanywa na wanajeshi wa serikali waloungwa mkono na Russia mwezi Januari, jeshi liliingia katika kijiji kilichpo jirani na kambi ya jeshi iliyoko katikati ya Mali na kuwakamata watu 25, wakiwemo watoto wanne. Ripoti inaeleza kwamba miili yao ilipatikana baaaye siku hiyo ikiwa imefungwa vitambaa machoni na majeraha ya risasi vichwani.
Amnesty International imesema katika taarifa tofauti mapema wiki hii kuwa ndege mbili zisizo na rubani zimeshambulia eneo la kaskazini mwa Mali na kuuwa watu wapatao 13 wakiwemo watoto saba walio na umri wa kati ya miaka miwili na 17. Mwanamke mjamzito alijeruhiwa na bomu mimba ilitoka siku kadhaa baada ya shambulio hilo, limesema shirika hilo.
Forum