Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:40

Watoto milioni 1.8 walazimika kuhama makwao kufuatia ghasia ukanda wa Sahel


Mali Jihadi Cattle Raids
Mali Jihadi Cattle Raids

Kuongezeka kwa ghasia nchini Mali, Burkina Faso na Niger, kumewalazimisha takriban watoto milioni 1.8, kuhama makazi yao, likiwa ongezeko mara tano, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, shirika la hisani Save the Children, lilisema Alhamisi.

Shirika hilo lisilo la kiserikali lilihesabu idadi ya watoto waliohama makazi yao katika nchi tatu za Sahel kwa kuangazia takwimu za Kamshina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), serikali za kitaifa na Shirika la kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Utafiti huo uligundua kwamba idadi ya watoto waliolazimika kuhama makazi yao iliongezeka kutoka 321,000 mwaka wa 2019 hadi milioni 1.8 leo.

“Mzozo huu uliopuuzwa sana katika kanda ya Sahel ya kati bado unasalia kuwa moja ya majanga mabaya ya kibinadamu duniani, na kuufanya kuwa mbaya zaidi kwa sababu ni mzozo wa watoto unaokumba kundi la watu wenye umri mdogo zaidi duniani,” alisema Vishna Shah, mkurugenzi wa kikanda anayehusika na utetezi na kampeni kwenye shirika la Save the Children.

Ivory Coast, ambayo ilimaliza vita vyake vya wenyewe kwa wenyewe nwaka 2011, pia imeathiriwa na kuenea kwa ghasia katika kanda ya Sahel, Save the Children ilisema.

Mizozo katika nchi jirani za Burkina Faso na Mali imesababisha ongezeko, mara kumi na mbili, la watoto wanaotafuta hifadhi Ivory Coast, kutoka watoto 2,450 mwishoni mwa 2022 hadi 29,700 hivi sasa.

Forum

XS
SM
MD
LG