Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:35

Takriban wanamgambo 40 wa al- Shabab wauawa Somalia


Wanajeshi wa Somalia wakiwa katika gari la kijeshi huko Mogadishu Machi 15, 2024. Picha na Hassan Ali ELMI / AFP.
Wanajeshi wa Somalia wakiwa katika gari la kijeshi huko Mogadishu Machi 15, 2024. Picha na Hassan Ali ELMI / AFP.

Serikali ya Somalia imesema kuwa oparesheni mpya ya kijeshi dhidi ya kundi la al- Shabab imesababisha takribani vifo vya wanamgambo 40 katika mkoa wa Lower Shabelle.

Katika taarifa ya wizara ya habari, Utamaduni na Utalii, serikali imesema operesheni hiyo ilifanywa na jeshi la Taifa la Somalia na “Washirika wa Kimataifa” ikitaja kuhusika kwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na nchi zinaoiunga mkono jeshi la Somalia.

Oparesheni hiyo imefanyika katika viijiji vya Baldooska na Baghdad, takribani kilimenta 30 kaskazini mwa Mogadishu. Taarifa hiyo haikusema lini oparesheni hiyo ilipofanyika, lakini vyanzo vimesema ilitokea Jumatatu jioni.

Oparesheni hiyo imefanyika baada ya majeshi ya serikali kupokea taarifa kuwa wanamgambo wamekuwa wakijiandaa kufanya mashambulizi dhidi ya raia, taarifa hiyo imesema.

Chombo cha habari chenye uhusiano na Al-Shabab kimeripoti pia juu ya shambulio hilo. Na toavuti moja ya al- Shabab imedai kwamba shambulio katika kijiji cha Baghdad limeua watu 18, wakiwemo watoto saba.

Chombo cha habari cha Al- Shabab pia kimecha picha za watu wanaodaiwa kuwa wameuawa katika shambulio hilo. VOA haikuweza kuthibitisha kwa njia huru madai ya mauaji hayo yaliyotolewa na pande mbili.

Alipohojia na idhaa ya Kisomli ya VOA, naibu waziri wa habari Abdirahman Yusuf al-Adala amesema serikali inakagua ripoti za majeruhi miongoni mwa raia.

Afisa wa Somalia ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia Idhaa ya Kisomali ya VOA kuwa oparesheni zote za anga na nchi kavu zimekuwa zikiwalenga wapiganaji wa al- Shabab tangu Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG