Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:03

Mapigano yauwa watu 42 Chad


Mapigano baina ya jamii mbili mashariki mwa Chad, yameuwa takriban watu 42, wizara ya usalama wa umma imesema leo hii, katika eneo hilo la jangwani la nchi ya Sahel, ambalo hukumbwa mara kwa mara na migogoro ya ardhi.

Wizara haikuweka wazi kabisa juu ya wanaohusika katika mapigano ama kwa muda gani yalifanyika, lakini eneo hilo mara kwa mara hushuhudia mapigano baina ya wakulima na wafugaji na makundi mengine kuhusu ardhi.

Wizara kupitia taarifa yake imeeleza kwamba mapigano yamesababisha watu 175 kukamatwa katika eneo la tukio, ambapo sehemu kubwa ya kijiji cha Tileguey, katika jimbo la Ouddai, ilichomwa moto na watu waliokuwa na silaha.

Waziri wa usalama wa umma Mahamat Charfadine Margui, ameiambia AFP kwa njia ya simu kwamba hali sasa ni shwari, lakini anaendelea kupatanisha pande zote.

Forum

XS
SM
MD
LG