Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:42

Watu 25 wauawa katika mapigano katika mji wa kaskazani mwa Darfur


Ramani ya Sudan inayoonyesha Kaskazini, Kusini na Magharibi mwa Darfur
Ramani ya Sudan inayoonyesha Kaskazini, Kusini na Magharibi mwa Darfur

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi hasimu cha wanamgambo yaliua raia 25 katika mji wa kaskazini mwa Darfur wa El-Fasher, kundi la wanasheria wanaotetea demokrasia lilisema Jumanne.

Mji huo na vijiji vya karibu vimekumbwa na” mashambulizi ya kiholela na ya anga” kwa siku kadhaa, kulingana na wanasheria wa dharura, ambao wamekuwa wakichunguza vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya raia tangu mapigano yalipoanza mwaka mmoja uliopita kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).

Wakati vita hivyo vikiingia mwaka wake wa pili, Umoja wa mataifa na Marekani zimeonya juu ya kuzorota kwa amani huko El-Fasher, mji mkuu wa mwisho wa jimbo la Darfur ambao hauko tena chini ya udhibiti wa RSF, na kwamba kutakuwa janga kwa maelfu ya watu ambao tayari wanateseka kutokana na janga la kibinadamu.

El-Fasher pia inafanya kazi kama kitovu kikuu cha misaada ya kibinadamu katika eneo kubwa la magharibi la Darfur, ambalo ni makazi kwa karibu robo ya raia milioni 48 wa Sudan na eneo la ghasia kali wakati huu na wakati wa mizozo ya awali.

Forum

XS
SM
MD
LG