Kikosi hicho cha SADC kilipeleka wanajeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini mwezi Disemba kusaidia serikali ya Kinshasa kudhibiti tena maeneo yaliyotekwa na waasi wa M23 mashariki mwa nchi.
Kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi wa Afrika Kusini, Tanzania na Malawi.
“Tukio hili la kusikitisha lilitokea baada ya kombora la adui kuanguka karibu na kambi ya wanajeshi hao,” taarifa ya kikosi cha SADC ilisema.
Haikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo.
Forum