Katika uamuzi wa kushangaza, mahakama ya uchaguzi ilimpa haki rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 81, ambaye atawania kwa tikiti ya chama cha uMkhonto we Sizwe (MK), chama kipya cha upinzani ambacho kinaonekana kuwa tishio kwenye uchaguzi wa Mei 29.
“Uamuzi wa tume ya uchaguzi umewekwa kando,” mahakama iliandika katika uamuzi ambao AFP imeuona.
Uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkali tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994 na kuwepo kwa Zuma katika kampeni inaweza kuwa kichocheo cha ushindani huo.
Kikitegemea umaarufu wa Zuma, chama cha MK kinatarajiwa kugawana kura na chama tawala cha African National Congress, makao ya kisiasa ya rais huyo wa zamani.
Hiyo inaweza kupelekea kura za ANC kushuka chini ya asilimia 50 kwa mara ya kwanza tangu 1994.
Chama cha MK kimepongeza uamuzi wa mahakama kama “ushindi” dhidi ya kile umesema zilikuwa juhudi zinazoongozwa na ANC kutaka kukitenga.
Forum