Maandamano yaliyopewa jina la "People's March" yalianza kutoka uwanja wa Franklin na kupita kati kati ya jiji la Washington hadi uwanja mkubwa mbele ya makumbusho ya Lincon.
Maelfu ya waandamanaji washiriki katika maandamano ya People's March 2025
Maelfu ya watu wengi wao wanawake waliandamana mjini Washington Jumamosi Disemba 18, 2025, kulalamika dhidi ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump, na kutoa ujumbe wa kulinda haki zote za kiraia na kibinadamu.
Huldah Momanyi Hiltsley aliweka historia hapo Novemba 5 alipokua mhamiaji wa kwanza mzaliwa wa Kenya kuchaguliwa mbunge wa jimbo la Minnesota.
Rais Azali Assoumani wa Comoro amejeruhiwa kidogo baada ya kushambuliwa na mtu aliyemkaribia na kumchoma kisu kichwani.
Rais wa korea kusini Yoon Suk Yeol amesisitiza umuhimu wa jukumu la Afrika katika uzalishaji wa madini na kueleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano wa uchimbaji madini na biashara kati yao.
Jopo la wajumbe wa mahakama moja mjini New York, Alhamisi limempata na hatia rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa mashtaka 34 ya kugushi hati zake za biashara.
Rais Joe Biedn ametia saini Jumatano mswada ambao utaweza kupiga marufuku app maarufu ya TikTok kutumika kote nchini, hivyo kuongeza kitisho dhidi ya biashara za kampuni hiyo Marekani.
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa vikosi vya usalama vya Comoros kutotumia nguvu vinapopambana na waandamanaji wenye hasira, baada ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kumtangaza Rais Azali Assoumani mshindi wa uchaguzi wa Januari 14.
Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza Jumanne Januari 9 kwamba, inathibitisha matokeo ya uchagzui wa rais yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi CENI, yanayompatia ushindi Felix Tshisekedi
Wagombea kiti cha rais katika uchaguzi wa Disemba 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanazunguka nchi nzima kunadi siasa na sera zao kukiwepo na idadi kubwa ya wafuasi wanaojitokeza kwa mikutano yao.
Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa Jumuia ya Kimataifa na vyombo vya habari kutosahau mzozo wa kibinadamu mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati ghasia dhidi ya wanawake na wasichana zikiripotiwa zinaongezeka.
Utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani unaishinikiza Israel kuchukua tahadhari kuzuia mauwaji ya raia wa Palestina wakati mapigano mapya yameanza Juujmapili kati kati ya Ukanda wa Gaza.
Mamia ya wanajeshi wa Kenya wameondoka kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili mchana, ikiwa ishara ya kuanza kuondoka kwa kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki, baada ya Kinshasa kukata kuongeza muda wake ili kupambana na kundi la M23.
Rais Joe Biden wa Marekani amesema kwamba ameridhika kwa dhati kwamba baadhi ya mateka walochukuliwa na wanamgambo wa Hamas walipoishambulia Israel Oktoba 7 watakua huru karibuni kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Israel na Hamas.
Maafisa wa afya wa Gaza wanasema ukosefu wa mafuta imesababisha kusitishwa kazi kwenye hospitali kadha Gaza kaskazini ambako watoto watano wachanga wamefariki Jumapili pamoja na wagonjwa 7 walokua mahtuti baada ya mashini za kuwapa oxygen kusita kufanya kazi.
Wanajeshi wa Israel wamepambana vikali na wapiganaji wa Hamas Jumapili karibu na hospitali kubwa kabisa ya Gaz, Al Shifa ambako maelfu ya watu wamekwama.
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepinga Jumatatu usiku mswada wa azimio ulowasilishwa na Rashia unaolaani ghasia zinazoendelea Mashariki ya Kati.
Rais Joe Biden wa Marekani amesisitiza wakati wa mkutano na waandishi habari akiwa Hanoi, Vietnam kwamba hana nia ya kuidhibiti China, wakati nchi hizi mbili zinazidi kutofautiana juu ya masuala ya biashara, usalama na haki za binadam.
Pandisha zaidi