Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 11:38

Rais Azali wa Comoro ajeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu


Azali Assoumani ahutubia kikao cha 78 cha kila mwaka cha Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa.
Azali Assoumani ahutubia kikao cha 78 cha kila mwaka cha Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa.

Rais Azali Assoumani wa Comoro amejeruhiwa kidogo baada ya kushambuliwa na mtu aliyemkaribia na kumchoma kisu kichwani.

Msemaji wa ikulu amethibitisha tukio hilo na kusema Rais Azali yuko salama kwani jeraha aliyopata ni ndogo.

Maafisa wa ikulu wanasema mtu aliyemshambulia ambae ni afisa wa polisi anashikiliwa na kikosi cha ulinzi wa rais ili kuhojiwa.

Rais Azali alikua amekwenda kutoa rambi rambi zake kwa familia ya mzee moja katika mji wa Salimani kati kati ya kisiwa cha Ngazija karibu na mji mkuu wa Moroni..

Hasira na upinzani dhidi ya utawala wa kiongozi wa visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi umeongezeka tangu alipomteuwa kijana wakemwezi wa Julai kuwa katibu mkuu wa serikali akiwa na mamlaka makubwa kuliko jinsi katiba inavyoeleza.

Azali mwenye umri wa miaka 65 mtawala wa zamani wa kijeshi alichukua madaraka kupitia mapinduzi 1999, na kurudi tena Februari 21, 2016.

Polisi wa kupambana na ghasia wakipiga doria baada ya ghasia mjini Moroni
Polisi wa kupambana na ghasia wakipiga doria baada ya ghasia mjini Moroni

Alibadilisha katiba na kuchaguliwa kwa mhula wa tatu mwezi Januari 2024 baada ya uchaguzi ulozusha upinzani mkubwa na ghasia za siku mbili.

Forum

XS
SM
MD
LG