Kufuatana na matokeo hayo rasmi yaliyotangazwa na mahakama hiyo, Tshisekedi amepata asili mia 73.47 za kura, akifuatiwa na mpinzani wake mkuu Moise Katumbi aliyepata asili mia 18.08 za kura.
Martin Fayulu mgombea aliyeshindwa na Tshisekedi wakati wa uchaguzi wa 2018 alichukua nafasi ya 3 akipata asili mia 4.92 za kura.
Uwamuzi huo ni wa mwisho na hauwezi kubadilishwa, wala kukatwa rufaa kulingana na katiba ya Congo.
Uwamuzi huu ulitangazwa baada ya mahakama kusikiliza na kutupilia mbali kesi mbili za malalamiko, moja iliyowasilishwa na mgombea moja kati ya 18 walogombania wa kiti cha rais hapo Disemba 20, Theodore Ngoyi, aliyepinga matokeo ya awali yaliyotangazwa na CENI.
Kesi ya pili iliwasilishwa na raia ambae mahakama imesema hakua na misingi ya kisheria kufikisha mashtaka kwani hakua mgombea kiti cha rais.
Mpinzani mkuu wa Tshisekedi Katumbi na wagombea wengine wa upinzani walikata kuwasilisha mashtaka wakisema hawana imani na mfumo wa mahakama.
Forum