Maandamano yaliyopewa jina la "People's March" yalianza kutoka uwanja wa Franklin na kupita kati kati ya jiji la Washington hadi uwanja mkubwa mbele ya makumbusho ya Lincon.
Waandamanaji walikusanyika pamoja na kusikiliza hotuba kutoka viongozi wa asasi mbali mbaloi za kiraia kuhusiana na kulinda demokrasia, haki za wanawake hadi haki za uzazi na usawa wa kijinsia na haki za mashoga.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Analilia Mejia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Popular Democracy, amesema maandamano hayo yana lengo la kuwaleta pamoja wanaharakati na waungaji mkono ili kuwakumbusha masuala muhimu ya demokrasia yanayokabiliwa na kitisho chini ya utawala mpya.
Anasema ujumbe muhimu ni kuhakikisha vita vinaendelea na mageuzi ya kweli yanapatikana baada ya vita vya muda mrefu.
Maandamano ya mwaka huu yakupinga kuapishwa kwa Trump yamekua madogo zaidi kuliko myale yaliyofanyika wakati wa awamu yake ya kwanza 2017, kwa sehemu fulani ni kutokana na vuguvugu la kutetea haki za wanawake Marekani limegawika baada ya Trump kumshinda makamu rais Kamala Harris mwezi Novemba.
Trump aliwasili Washington Jumamosi na ameanda karamu katika klabu yake ya mchezo wa Golf mjini Sterling, Virginia na atahudhuria mkutano wa ushindi wake katika uwanja wa Capitol One Arena, Washington siku ya Jumapili ulopewa jina la "Make Amerika Great Again".
Forum