Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:42

UN yatoa wito wa kuwepo utulivu Comoros baada ya upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais


Wafuasi wa upinzani wakiharibu bango la Rais Azali Assoumani mjini Moroni wakati wa maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa Januari 14, 2024.
Wafuasi wa upinzani wakiharibu bango la Rais Azali Assoumani mjini Moroni wakati wa maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa Januari 14, 2024.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa vikosi vya usalama vya Comoros kutotumia nguvu vinapopambana na waandamanaji wenye hasira, baada ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kumtangaza Rais Azali Assoumani mshindi wa uchaguzi wa Januari 14.

Hali ya wasi wasi imeenea katika visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi Jumatano, baada ya polisi kupambana na waandamanaji katika miji mbali mbali, kuanzia Jumanne usiku baada ya matokeo kutangazwa.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika mji mkuu wa Moroni ili kutawanya waandamanaji na kufunga barabara kuu zote za miji muhimu ya visiwa hivyo huku wananchi wakifunga barabara kuzia wanajeshi kuingia katika miji yao.

Polisi na wanajeshi wa Comoros wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Moroni baada ya kuzuia maandamano ya upinzani.
Polisi na wanajeshi wa Comoros wakipiga doria kwenye mji mkuu wa Moroni baada ya kuzuia maandamano ya upinzani.

Tume Huru ya Uchaguzi ya Comoro, CENI, ilitangaza matokeo rasmi ya awali Jumanne usiku, yanayompatia Rais Assoumani, mwenye umri wa miaka 65, ushindi wa asili mia 62.9 na kumrudisha madarakani kwa mhula wanne.

Mkuu wa Haki za Binadam wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema Jumatano kwamba, “Mivutano baada ya uchaguzi ikiongezeka ni muhimu kabisa kwa maafisa wa usalama kuhakikisha mazingira ya usalamaambayo Wakomoro, pamoja na wanasiasa wa upinzani, wanaweza kujieleza kwa njia huru na kutekeleza haki zao za kukusanyika kwa amani.”

Upinzani umetaka matokeo na kutaka uchaguzi ufutiliwa mbali, ukidai kwamba serikali imefanya wizi kwa kujaza masanduku ya kura na kura zinazompendelea Rais Assoumani.

Msemaji wa serikali Houmed Msaidie akizungumza na Shirika la Habari la AFP, ameulamu upinzani kwa kuanda maandamano na kusababisha ghasia.

Aliongezea kusema kwamba kuna watu walokamatwa lakini hakuweza kutaja ni watu wangapi walokamatwa.

Baadhi ya waandamanaji walivamia nyumba ya waziri mmoja wa serikali iliyopita na kutia moto huku waandamanaji wakifunga barabara kwa kutia matairi moto ili kuwazuwia wanajeshi kusonga mbele.

Wafuasi wa upinzani wakikiadi polisi na jeshi wanapoandamana mjini Moroni kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais hapo Januari 17, 2024 .
Wafuasi wa upinzani wakikiadi polisi na jeshi wanapoandamana mjini Moroni kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais hapo Januari 17, 2024 .

Abdelrahmane mkuu wa shule ya msingi anasema watu wanahofu kubwa kutokana na jinsi hali ilivyo kwa wakati huu.

“Hali iko mbaya kwa sababu ya serikali. Serikali ndio inabidi kutulinda pamoja na mali zetu, kwa maoni yangu. Wamekuja kutushambulia hapa shule ambako kuna wanafunzi. Wametumia gesi ya kutoa machozi. Wanawashambulia watu kiholela. Hali ni mbaya na inatia wasi wasi,” amesema Abdelrahmane

Polisi na maafisa wa kikosi maalum cha kupambana na ghasia wamepelekwa katika maeneo mbali mbali ya miji mikubwa ya visiwa hivyo kushika zamu na kuzia maandamano kufanyika. Watu kadhaa wanaripotiwa kujeruhiwa kwenye visiwa vya Nzwani na Mwali.

Upinzani unadai kwamba kumekuwepo na wizi wa kura hasa kukiwa na watu waloonekana kupitia video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijami ambayo Sauti ya Amerika haijawezi kuthiubitisha ikionesha wanawake wanawasili kwenye vituo vya kupiga kura na kujaza sanduku ya kura na vyeti vingi vya kura.

Forum

XS
SM
MD
LG