Baraza la wawakilishi la Bunge la Marekani lilipitisha mswada huo Jumamosi, uloambatanishwa na msaada wa kigeni kwa Israel, Ukraine na mataifa mengine siku ya Jumamosi.
Baraza la Senet liliidhinisha mswada huo Jumanne usiku, na kuwa kitisho kikubwa zaidi kwa TikTok tangu maafisa wa usalama wa Marekani kuanza kueleza wasi wasi wao kuhusu app hiyo mwaka 2020.
Chini ya sheria hiyo mpya, TikTok inalazimika kumtafuta mmiliki mpya katika muda wa miezi 9, la sivyo kupigwa marufuku Marekani.
Sheria inilazimisha Tiktok kufanya nini?
Kile tunachofahamu ni kwamba sheria hiyo mpya inampatia mmiliki wa Uchina wa Tiktoko, ByteDance miezi 9 kuiuza kwa Mmarekani. Ikishindwa kufanya hivyo itaisababisha kukabiliwa na athari kubwa.
App hiyo itapigwa marufuku kutumiwa na wateja wake wa Marekani kwa kutouzwa kwenye maduka ya app na kutoruhusiwa kuwekwa kwenye “kampuni za mitandao” zenye ushirikiano na program hiyo.
Hiyo ina maana itakua ni marufuku kupakua app hiyo kuanzia wakati huo na kuwasiliana na maudhi yake.
Chini ya sheria hiyo hata hivyo, Rais Biden anaweza kuongeza muda wa siku 90 baada ya muda wa kutakiwa kuuzwa wa Januari 19, 2025 umepita ikiwa ameona ishara za maendeleo za kampuni hiyo kuiuza Tiktok na hivyo kuipatia kampuini hadi mwaka mmoja kabla ya kupigwa marufuku hapa Marekani.
Nini msimamo wa Tiktok?
TikTok imetishia kiuwasilisha mashtaka dhidi ya sheria hiyo. Kwenye video iliyochapishwa kwenye mtandao, mkurugenzi mtendaji wa kampuni Shou Chew aliwambia wateja wake wa Marekani kwamba “Nina kuhakikishieni, hatuondoki hapa”
Kampuni hiyo inaamnini katiba ya Marekani inawalinda kutokana na kwamba utumiaji ukurasa wake unatokana na kifungu cha sheria cha haki ya kujieleza.
Katika taartifa, msemaji wa Tiktok ametaja sheria hiyo kwamba inakwenda “kinyume cha katiba” akiongeza kusema kwamba hiyo itawakera kabisa watumizi wake milioni 170 na biashara milioni n7 zinazotumia app hiyo.
Imefika vipi hapa
Inabidi kukumbuka kwamba kampuni kubwa ya teknolojia ya Uchina ByteDance ilinunua app mashuhuri ya karaoke Musical.ly mwaka 2017 na kuzindua huduma zake kama Tiktok.
Tangu waketi huo app hiyo imekua ikikaguliwa na maafisa wa usalama wa kitaifa wa Washington walokua na hofu kwamba kunauwezekano serikali ya Bejing inahusika na ikawa na ushawishi katika kampuni hiyo.
Licha ya wasi wasi huo TikTok ilizidi kupata umaarufu kufikia hivi sasa kuwa ni jukwa linalotumiwa na nusu ya wakazi wa marekani, ambapo theluthi moja ya vijana wa nchi wanapata habari zao kulingana na kituo cha utafiti cha Pew.
Vijana hao wanapinga vikali kupiugwa marufuku ukurasao wao mashuhuri wanaopata habari, muziki na mambo mengi ya kijamii, kibiashara na nafasi ya kujieleza kwa njia huru kabisa.
Waatalamu wa katiba wanasema sheria hiyo inaweza kuchukuliwa ni kuwanyima wateja wa Tiktok haki yao ya kujieleza na hatimae kufutwa na mahakama.
Forum